Sehemu Ya (158) : Kuna Mambo Flanii Flanii Lazima Na Muhimu Uyajue Kwenye Mapenzi..
'boyfriend’ na girlfriend' wanaelewana vizuri. Ni vigumu kupata mtu ambaye
mnaelewana kila jambo.
Sio lazima kama mwenzako anasapoti Arsenal na wewe usapoti Arsenal.
Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa, ili uweze kuishi vizuri na
mtu kama mume na mke ni vizuri kuwa mnaelewana kwenye masuala ya msingi na
mnashea vission moja ya maisha. Kati ya masuala ya msingi ambayo ni muhimu kuwa
kwenye ukurasa mmoja ni Matumizi ya fedha na kujamiiana. Haya ndio mambo makuu
mawili ambayo yanasababisha ndoa nyingi sana kuvunjika. Utajuaje matumizi ya
mtu ya fedha kama ndio wachumba na bado hamjaanza kuishi pamoja?
Ni rahisi, utakuwa unajua mwenzako anafanya kazi wapi, dadisi kwa watu
kuwa kazi kama anayofanya mwenzako ina mshahara kiasi gani pamoja na dili
nyingine anazofanya, ukishajua hilo anza kuchunguza matumizi yake, vitu
anavyonunua, mavazi anayovaa, gari analoendesha na mambo mengine kama hayo.
Kama matumizi yake yako juu kuliko kipato chake, jaribu kuongea naye na
kumshauri kuhusu matumizi yake.
Tunakuja kwenye swala ya kujamiiana, hili ndio jambo la pili ambalo
linaongoza kwa kusababisha mahusiano kuvunjika hasa kwa kizazi kipya. Miaka
kama 30 iliyopita, watu wengi walikuwa wanaoana wakiwa bado bikra. Jambo zuri
la kuoana mkiwa bado bikra ni kwamba wote mnaingia mkiwa hamna ujuzi na hamna
wasichana au wanaume wengine ambao umelala nao wa kulinganishe ujuzi wao na mke
wako au mume wako. Tatizo lipo siku hizi ambapo watu wanaoana wakiwa na ujuzi
tofauti (diffetent experience level) ndio maana michepuko imezidi.
Wanadamu tumezoea kulingalisha vitu, pale utakapoanza tu kulinganisha
utaalamu wa mwenzako na wanawake au wanaume wako wa zamani ndio utakapoanza
kumuona mwenzako hafai. Jitahidi kutolinganisha uhusiano wako na watu
waliopita, hamna watu wawili wanafanana kila kitu humu duniani. Kabla
sijamalizia, napenda kusisitizia kuhusu umuhimu wa mawasiliano, sio kupigiana
simu na kuandikiana message kwenye whatsapp, kutaneni mahali, wekeni simu zenu
mbali na sio unaangalia picha instagram wakati unaongea na mwenzako.
Tafuteni sehemu iliyotulia mara mbili kwa wiki mzungumze na kupanga
maisha yenu, usiogope wala kuona haya kuuliza swali lolote.
Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment