Sehemu Ya (58) : Dalili Za Penzi Linataka Kufa Huwa Ni Kama Za Malaria Tu.
Penzi huwa halidondoki na kufa ghafla kama Mgonjwa wa
Degedege na Beriberi, Penzi huwa
linakufa kwa Process zinazoonekana lakini
zinazodharaulika. Dalili za Penzi linalotaka Kufa huwa ni kama dalili za
Malaria, utaona tu dalili... Kichwa kitauma... Mwili utakuwa mzito na Homa...
Ukidharau ukanywa tu Panadol ndo watu huzidiwa na kufa ghafla.
Usidharau Ukiona Vimelea vya Penzi linaloumwa... Ukiona
Penzi lako lina Homa litafutie tiba Stahiki kabla hali haijawa tete na Chronic
likalazwa ICU na hatimaye kukata roho maana hutaamini macho yako kwamba
limekufa kwa ka-homa haka tuu!
Dalili za Homa Ya Penzi huwa ziko wazi ila tunazipuuziaga na
kuziona oya-oya...Kama unamjua Mpenzi wako utaona tu anavyochange na kuanza
kupata vipele vya baridi... Atabadilika anavyoongea na wewe... Attention
anayokupa si kama zamani... Visingizio kibao badala ya kuomba msamaha akikosea
na Communication inayoyumba-yumba kama Mlevi wa Wanzuki.
Usipotibu Penzi lenye Homa jiandae kwa Mazishi... Simple and
Clear... Kama Malaria isivyokubalika Africa, Usikubali Homa ya Penzi iue Mahaba
yako uliyonayo kwa Hubby Ake...Tibu Homa pale inapotokea usisubiri ulazwe ndo
utafute Kwinini.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment