Sehemu Ya (52) : Je, Unaijua Kanuni Watumiayo Ladies Mjini Ili Waolewe..?? Inaitwa T.M.U.
Unapokutana na COUPLE yenye Miaka takribani 10 wakiwa
wanapendana kama
wameoana jana, wakitaniana na kucheka pamoja, wakikusimulia
kuhusu utamu wa ndoa na jinsi walivyokutana mpaka walipoamua KWA HIARI YAO WOTE
WAWILI kwamba They are a Perfect Match na wanaweza kulisongesha Gurudumu la
maisha kwa pamoja... Inatia moyo, hata kama ulikuwa na Moyo Mgumu kama Farao,
uunajikuta unalainika na kutamani kuanza kusaka Mshenga!
INASIKITISHA SANA:
Unapoona Vijana ambao wamekaa pamoja katika Urafiki na
Uchumba kwa Miaka 9 na Mwanaume 'kadinda' kwa sababu anahisi MATCHING CONCEPT
ya Mke na Mme inamiss halafu Bishosti anahisi 'Anapotezewa Muda', na amechoka
kusimamia Send-Off za Wenziwe, akaamua kufanya 'Mchakato wa Kurasimisha Rasimu
ya Ndoa kwa kutumia Mimba' kwa Mfumo wa TMU (Tegesha Mimba Uolewe) na kwa
presha jamaa akaamua kukuoa kweli ili kuiwahi Mimba mtoto azaliwe ndani japo
alipatikana nje.
Maisha ya COUPLE hizi 2 ni Toooofautiiii kama Usingizi na
Kifo, na Ushauri utakaopewa kutoka kwa COUPLE hizi 2 ni CONTRADICTORY! Hawa
wako EDENI wanachuma matunda, na hawa wengine wako BOKO HARAM CAMP!
Acha Penzi likue lizae Ndoa Automatic, Usivundike Penzi
kabla halijaiva, Maembe ya Kuvundika huwa Si Matamu kama Yale yaliyoiva yenyewe
yakaanguka chini kama VIBWADE
Acha Penzi lizae Ndoa.... Nikiona Mimba Inazaa Ndoa
najisikia KUTETEMEKA mpaka nanena kwa lugha, Ohhhh rikabababaataratabaka
sayahatataraba rohobosita KANTANGAZE..
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter ,@KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment