Sehemu Ya (18) : Usikubali Kuingia Kwenye Uhusiano Na Mtu Mwenye Tabia Za Korea Kaskazini.


Watu Kama hao muda wote wanawaza Majaribio ya Nyuklia... Huwa hawako serious...

Leo anakwambia anakupenda, kesho anakwambia 'My ex called me, hata sielewi nifanye nini'. Kabla hujakaa sawa anakwambia am confused, my ex wants to marry me now halafu bado nampenda..

Mtu asiye na msimamo hafai kwa Relationship, we utatoa moyo wako kumbe yeye anafanya Majaribio, ex akirudi umetoswa... Kuwa makini na hawa watu, mijitu ambayo haijapona maumivu ya past relationships hawafai, ukijitoa mhanga kaa mkao wa kula au kuliwa, anything can happen anytime.


Etii.. Unamfumania Boyfriend wako na mwanamke mwingine, unamwambia achague, kati yako wewe na yule mwanamke, anakwambia umpe muda achague, kwa sasa hajui amchague nani.. na ulivyo mjinga kweli unampa muda eti akafikirie wa kumchagua, UNA AKILI WEWE?? Kama hajielewi sasa hivi kamwe usitegemee atajielewa hata umpe miaka 100..


 Girls, know ur standards, Mapenzi yasiwafanye muwe mapunguani kwa kushindwa kuona vilivyo wazi, Maandishi hamuoni hata Picha hamuelewei??? Ondoka, hapo huna nafasi, to him you are just an Option.

Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments