Sehemu Ya (19) : Unaweza Ukawa Na Ndoto Za Kumuoa Wema Sepetu Lakini Ukaishia Kwa Mange Kimambi.
Kuwa Rubani wa Ndege haimaanishi ndio utakuwa Rubani wa
Ndoa.. Unaweza kuwa Mwanajeshi tena Brigedia lakini kwenye Ndoa ukawa Kuruta 😂...
Mwanasheria unaweza kusimama kwenye Court kwa ustadi lakini kusimama ndani ya
ndoa ni zaidi ya Extended Jurisdiction!
Mapenzi sio Mchezo.... Maprofesa wanakuna Vipara... Formula
hakuna... Research zimebuma.. No Submission.... once U fall in Love heshimu
hisia kwanza Status & Personality baadae! Kijana naweza leo nikawa na ndoto ya kumuoa Miss World
lakini kesho nikaishia kudondokea Katika Penzi zito la Binti Afisa wanyamapori
Kitalu cha Kutunza NGIRI kule Mikumi 😂 That's Love!
Unaweza sema utamuoa Mrembo Engineer tena under eighteen
lakini ukaishia kupeleka Mahari kwa Bibi mstaafu wa Kiwanda cha Tumbaku
Morogoro,.. That's Love!
Wapo Warembo Very Selective na waliowahi kutamba kwamba
wataolewa na Vijana MA-handsome na Ma-tall lakini mwisho wa siku wakajikuta
wamezama kwenye mapenzi mazito na Vibabu vistaafu Tanganyika Packers 1992,.. yaani Kibabu ngozi imekauka .. Babu
hapigwi busu mpaka apakwe Mayyonise.😂.... That's Love!
MAPENZI KWELI HISIA... Huwezi jua, TUHESHIMU WENZETU.
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Twitter @KissToTheLadies
WhatsApp +255 715 758 021
Post a Comment