Sehemu Ya (126) : Ladies, Maamuzi Yako Ndio Maumivu Yako... Au Furaha Yako.

WADADA MNISAMEHE KIDOOOGO!..

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!.

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi wa kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakini upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.
Kweli huenda we ni mtoto wa kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja, anaye vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anayeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!.

Una mpuuza na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambaye kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambaye ni baba fulani na ni mume wa fulani kisa tu ana pesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda kutoka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?..

Dada maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake.. Mwaka wa ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanaume ?.Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume wa kawaida lakini leo wana mafanikio? Kwa nini usiige?


Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanaume yeyote mwenye akili timamu,

Watumiaji Wa "Android" Unaweza Download App Yangu Hapo Chini
Ili Kupata Posts Zangu Kirahisi Zaidi Kwenye Simu Yako.http://www62.zippyshare.com/d/FvrvpQQg/31722/xxlbongotz.apk
Pia Unaweza Nifollow:
Facebook , Instagram , Snapchat , Twitter @KissToTheLadies 
WhatsApp +255 715 758 021

No comments